Karibuni kwa shule Uswidi Nairobi(SSN).
Tupo kwenye makutano ya barabara ya Ngong’ ( Ngong’ road) na ya Makindi ( Makindi road) pempeni mwa klabu ya Impala (Impala sports club) Nairobi. Tunawapa elimu bora wanafunzi kutoka eneo la Scandinavia waliomo nchini Kenya.
Shule inafuata maagizo ya elimu kutoka Uswidi na masomo mengi yanafunzwa kwa Kiswidi. Tunashughulikia wanafunzi kutoka miezi kumi na minane (chekechea) hadi kufuzu baada ya elimu ya sekondari (miaka 18 hadi miaka 19). Idadi ya wanafunzi ni kasoro au kuzidi 150 ambapo nusu yao ni chekechea na nusu nyingine sekondari.
Kwa sababu tunatambulika na kuegemea mrengo wa elimu kutoka Uswidi, alama za masomo zinatambuliwa na vyuo vikuu vya Uswidi pamoja na idara ya elimu pia. Hamna kutafsiri kwa alama mwanafunzi ahamiapo Uswidi.
Tuna mabweni ya wanafunzi wa sekondari ya juu pekee,yanayowezesha wanafunzi wageni kupata mwaka mmoja wa uzoefu wa Afrika mashariki na kufaidi kuendelea moja kwa moja na madasa yao ya awali Uswidi. Wanafunzi ambao huchukua mwaka mmoja katika maeneo mengine ya dunia kama vile Uingereza, Marekani au Uastralia huwa ni sharti waelimike kisekondari tena Uswidi ili wakubalike vyuoni Uswidi.
Hivi sasa, tunawakubali tu wanafunzi ambao angalau mzazi wao mmoja ni msemi wa lugha ya Kiswidi nyumbani ingawa Kiingereza ni mojawapo wa lugha ya mawasilano ya kila siku shuleni mwetu.
Kwa taarifa zaidi au maswali, tafadhali usisite kuwasiana nasi;